NECTA yasua kizaazaa Zanzibar

Baadhi ya wazee ambao walishiriki katika kongamano la kutathmini matokeo ya mtihani yaliotangazwa na baraza la elimu Tanzania (NECT) ambalo limewafutia jumla ya wanafunzi 3303 kwa madai ya udanganyifu wengi wao wakielezwa ni kutoka Zanzibar

Na Ally Saleh

Wiki iliyopita ilikuwa ni kubwa kwa habari za matokeo ya mtihani wa Kidato cha Nne kwa taifa lakini zaidi kwa upande wa Zanzibar. Ni hizo zilitikisa bahari ya Hindi hadi visiwa vikawa vinatetemeka. Ilibidi Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) Joyce Ndalichako afanye ziara ya kuja Zanzibar kuelekezea nini kimejiri mpaka yakatokea yaliotokea ambayo wazee na wanafunzi bado hawajaamini. Continue reading

Wafanyakazi wanafaa kulindwa- Balozi Seif

MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALI IDDI AKILIFUNGUA KONGAMANO LA KITAIFA KUADHIMISHA MIAKA 10 YA CHAMA CHA WALIMU ZANZIBAR. SHUGHULI HIYO ALIIFANYA KWA NIABA YA RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DR. ALI MOHD SHENI HAPO UKUMBI WA ZAMANI WA BARAZA LA WAWAKILISHI KIKWAJUNI MJINI ZANZIBAR.

Vyama vya Wafanyakazi vinapaswa kupatiwa haki na fursa zote zinazostahiki katika kuruhusiwa kufanya kazi zake kikamilifu bila ya bughudha ya aina yoyote. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohd Sheni alitoa kauli hiyo wakati akifungua Kongamano la kuadhimisha miaka 10 ya Chama cha Walimu Zanzibar liliofanyika katika Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi uliopo Kikwajuni Mjini Zanzibar. Continue reading

Siasa sio mradi wa biashara- Maalim Seif

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa (MKUAJI) katika shehia ya Mtoni Kidatu, Wilaya ya Magharibi Unguja. Kushoto kwake ni Mwakilishi wa Jimbo hilo Nassor Ahmed Mazrui

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amesema siasa sio uwanja wa biashara bali ni fursa ya kuwatumikia wananchi, hasa katika majimbo ya uchaguzi. Alisema kwa kuzingatia kuwa kuingia katika siasa ni fursa ya kuwatumikia wananchi, viongozi wa kuchaguliwa lazima wajenge utaratibu wa kushikikiana kwa karibu katika kufanyakazi za kuwakomboa wananchi kutoka katika umasikini. Continue reading